Tutauwasha moto kama kawaida ligi ikirejea - Tshabalala

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jun 2020
Tutauwasha moto kama kawaida ligi ikirejea - Tshabalala

Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesema kikosi chao kinafanya maandalizi kabambe kuweza kurejea dimbani wakiwa katika ubora wao uliozoeleka

Tshabalala amewahakikishia mashabiki wa Simba kuwa wataendeleza pale walipoishia kwenye mchezo wao wa mwisho kabla ya ligi kusimama

Beki huyo mahiri wa kushoto, amesema kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha wanatetea ubingwa pamoja na kutwaa taji la FA

Aidha, ameongeza kuwa wamepokea kwa mikono miwili uamuzi wa ligi kuchezwa nyumbani na ugenini na kuwa utaratibu huo ndio uliokuwa ukitumika siku zote hivyo hautawasumbua

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi uwanja wa Mo Simba Arena wakijiandaa na mchezo wa kwanza wa ligi ambao utapigwa Juni 14 dhidi ya Ruvu Shooting

Upo uwezekano mkubwa mabingwa hao wa nchi watacheza angalau mchezo mmoja wa kirafiki wiki ijayo kabla ya kukumbana na Ruvu Shooting

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’