Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema mazoezi anayowapa wachezaji wake yatasaidia kuwaweka tayari kurejea katika mikiki mikiki ya ligi kuu mpango wao wa kwanza ukiwa kutetea ubingwa
Sven amesema miezi miwili ambayo wachezaji walikaa nyumban imeathiri utimamu wao na hivyo benchi lake la ufundi kuandaa program maalum ambazo zitawaimarisha
"Ratiba nimeiona, ukiniambia kuwa kwa sasa tupo tayari kucheza nitakwambia hapana, sababu wachezaji hawana utimamu wa mwili. Kwa hizi wiki mbili zilizobaki kabla ya ligi kurejea zitatusaidia kutuweka vizuri na jambo zuri ni kwamba asilimia kubwa wachezaji wote wako kikosini isipokuwa wawili tu," Sven aliiambia tovuti ya klabu ya Simba
Sven amesema ataendelea na utaratibu wa kubadili program za mazoezi ili kuhakikisha wachezaji wanakuwa tayari kushuka dimbani Juni 14 kuumana na Ruvu Shooting
Wiki iliyopita Simba ilianza na mazoezi ya nguvu, lakini kuanzia juzi, wamekuwa walifanya mazoezi ya kucheza mpira zaidi