Senzo amuondoa Shonga usajili Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jun 2020
Senzo amuondoa Shonga usajili Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amemaliza uvumi unaomuhusu mshambuliaji wa Orlando Pirates Justine Shonga anayehusishwa na mabingwa hao wa nchi

Senzo amesema kuwa mpaka sasa Simba bado haijaanza michakato ya usajili wa wachezaji wapya, lakini pia nyota huyo kutoka Zambia sio miongoni mwa wachezaji walio kwenye mipango yao

"Nimeziona taarifa nyingi zinazomuhusisha mchezaji huyo (Shonga) na klabu yetu. Nafahamu wakati huu kuelekea usajili mambo mengi yanaandikwa kwenye magazeti. Lakini Simba hatujaanza usajili wa wachezaji wapya, bado dirisha la usajili halijafunguliwa

"Kwa sasa tunahakikisha tunamalizana na wachezaji ambao tutaendelea nao msimu ujao. Shonga ni mchezaji mzuri lakini hatukuwahi kuwa na mpango wa kumsajili kwani tunao washambuliaji wanaofanya vizuri hapa," alisema Senzo

Aidha, Bosi huyo raia wa Afrika Kusini, amesisitiza kuwa kikosi chao kiko imara hivyo hawatarajii kufanya usajili mkubwa pale dirisha la usajili litakapofunguliwa

Amesema mapendekezo waliyopewa na kocha Sven Vandenbroeck ni kwa ajili ya kuboresha sehemu chache zenye mapungufu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’