Beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema jitihada, juhudi binafsi, ushirikiano na wachezaji wengine pamoja na kufuata maelekezo anayopewa na Walimu ndio siri mafanikio yake kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara
Akiwa kwenye msimu wake wa tano na Simba, Tshabalala ni miongoni mwa wachezaji ambao wamenyesha viwango vya hali ya juu sana msimu huu
Pamoja na kuwa ni beki, amehusika katika mabao manne ya Simba kwenye ligi msimu huu
Aidha licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Gadiel Michael aliyetua kutoka Yanga, Tshabalala ameendelea kuaminiwa na kuwa chaguo la kwanza kwenye nafasi ya ulinzi upande wa kushoto
"Nimekuwa nikifanya mazoezi kwa jihudi, nafuata maelekezo ya walimu na nashirikiana vizuri na wenzangu. Pia nimejiwekea malengo ya kuhakikisha napiga hatua kila msimu," amesema nahodha huyo msaidizi ambaye tangu mwaka 2017 ana kazi ya kuinua mataji ambayo Simba imekuwa ikishinda