Simba yapania kutangaza ubingwa baada ya mechi nne

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jun 2020
Simba yapania kutangaza ubingwa baada ya mechi nne

Vinara wa ligi kuu Simba ambao ndio mabingwa wa nchi hii kwa misimu miwili iliyopita, Simba watamaliza kampeni ya kusaka ubingwa wa tatu ugenini kwenye mchezo wa mwisho Julai 26 dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa uwanja wa Ushirika, Moshi

Lakini wakati huo huenda wababe hao wa soka ukanda wa Afrika Mashariki watakuwa wameshatwaa ubingwa na mchezo huo utakuwa wa kukamilisha ratiba tu

Simba imeweka mkakati wa kuhakikisha inashinda michezo yote minne ya mwanzo ligi itakaporejea Juni 13

Ruvu Shooting itakuwa klabu ya kwanza kuujaribu 'mziki' wa mabingwa hao watetezi katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa Juni 14

Juni 20 Simba itarejea tena katika uwanja huo kuikabili Mwadui Fc, katika mchezo ambao utazikutanisha timu hizo kwa mara ya tatu msimu huu

Mechi nyingine mbili zitakazofuata zitakuwa mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons

Simba itaumana na Mbeya City Juni 24 isha kurejea tena jijini Dar es salaam kucheza na Azam Fc mchezo wa kombe la FA

Itarudi tena Mbeya Julai mosi kuifuata Tanzania Prisons

Ushindi katika michezo hii minne huenda utaihakikishia Simba ubingwa wa tatu mfululizo

Baada ya mchezo wa Tanzania Prisons, Simba itaelekea Mtwara kuifuata Ndanda FC

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’