Kiungo wa Simba Ibrahim Ajib amemaliza adhabu aliyokuwa amepewa na kocha Sven Vandenbroeck na kuruhusiwa kuingia kambini leo
Wiki iliyopita, Ajib alishindwa kuungana na wenzake kambini baada ya kuchelewa kuripoti mazoezi tukio lililomkera Sven ambaye aliagiza nyota huyo asiruhusiwe kuingia kambini
Hata hivyo Sven alisema adhabu ya nyota huyo imemalizika mwishoni mwa wiki na leo ataruhusiwa kuingia kambini
Inaelezwa Ajib alipata changamoto ya kuwahi mazoezini Alhamisi iliyopita, ikidaiwa kuwa nyota huyo amehamia Chanika yalipo makazi yake mapya
ADVERTISE HERE