Kahata afunguka mkakati wa ubingwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jun 2020
Kahata afunguka mkakati wa ubingwa Simba

Kiungo fundi wa Simba Francis Kahata alirejea nchini juzi baada ya jitihada za ziada kufanikiwa kumchomoa huko Kenya ambako changamoto ya corona imesababisha nchi hiyo kuwa imefunga mipaka

Kahata alianza mazoezi jana, leo akiendelea kujifua na wachezaji wengine ambao walianza program za mazoezi tangu Jumatano iliyopita

Nyota huyo amesema wakati yuko Kenya alikuwa akifanya mazoezi kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na benchi la ufundi

Hata hivyo, Kahata amesema kama timu wanahitaji kujifua kukaa sawa tayari kwa mikiki mikiki ya ligi inayorejea Juni 13, Simba ikitarajiwa kushuka dimbani Juni 14 kuikabili Ruvu Shooting

Kahata amesema michezo ya mwanzo haitakuwa rahisi kwa timu zote kutokana na ukweli kuwa wamekaa muda mrefu bila ya kucheza mpira

"Michezo ya kwanza haitakuwa rahisi, wajua miezi miwili bila ya kucheza mpira ni mingi sana. Timu zitaanza taratibu lakini nadhani baada ya michezo mitatu tutakuwa sawa. Kama timu tuko vizuri na malengo yetu ni kutetea ubingwa. Timu yetu inaundwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa matumani ya kutetea ubingwa wetu wa ligi na kunyakua taji la FA ni akubwa" alisema Kahata baada ya kutua kambini

Simba inaendelea na mazoezi katika uwanja wake wa Mo Simba Arena

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’