Ligi Kuu ya Vodacom inarejea rasmi Juni 13 kwa mechi mbili kupigwa
Mapema leo, Bodi ya Ligi iliweka hadharani ratiba ya ligi kwa mechi zilizobaki ambazo zitafikia tamati Julai 26
Mabingwa watetezi ambao ndio vinara wa ligi hiyo, Simba wataanzia nyumbani Juni 14 wakiikaribisha Ruvu Shooting
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Juni 20 katika uwanja wa Taifa
Simba itakamilisha mchezo wa tatu mwezi Juni kwa kusafiri mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City Juni 24
Mchezo utakaofuata ni wa kombe la FA dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Juni 27 halafu mabingwa hao wa nchi watasafiri mkoani Mbeya tena kuifuata Tanzania Prisons, Julai 01
Ratiba kamili ya michezo yote itapatikana kwenye ukurasa wa ratiba
ADVERTISE HERE