Hiyo ni kauli ya nyota wa klabu ya Simba ambao leo asubuhi waliendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa kwa mikiki mikiki ya ligi kuu pamoja na kombe la FA
Taji la ligi kuu ni kama liko kibindoni tayari lakini mabingwa hao wa nchi wamepania 'kusepa' na mataji yote msimu huu
Wakati wakiwa wamepangwa kucheza na Azam Fc kwenye mchezo wa robo fainali ya FA, Simba inaweza kukutana na watani zao Yanga kama wote watashinda michezo yao ya robo fainali Yanga ikitarajiwa kucheza na Kagera Sugar
Kocha Mkuu wa mabingwa wa nchi hii Sven Vandenbroeck amesema wameweka mkakati wa kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo akiwataka Wanamsimbazi wasubiri mambo mazuri kutoka kwa timu yao


ADVERTISE HERE