Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, amesema Serikali imeruhusu ligi ambazo zilikuwa zikichezwa kwa utaratibu wa nyumbani na ugenini, zinaweza kurejea kupitia utaratibu huohuo
Dk Abbas ametoa kauli hiyo leo na kuondoa mapendekezo ya awali ambapo mikoa ya Dar es salaam na Mwanza ingetumika kumalizia mechi zilizobaki
Mechi za Ligi Kuu na Kombe la FA zingechezwa jijini Dar es salaam wakati mechi za Ligi Daraja la kwanza zingechezwa mkoani Mwanza
"Serikali inaruhusu ligi za soka ambazo kikanuni zinatakiwa kucheza nyumbani na ugenini, utaratibu huo wa nyumbani na ugenini badala ya kituo kimoja uendelee kutumika, " amesema Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara Ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo
Aidha Serikali pia imeruhusu mashabiki kuingia uwanjani kwa angalau nusu ya uwezo wa viwanja pale inapobidi
Bodi ya Ligi inatarajiwa kutoa ratiba ya michezo iliyobaki siku ya kesho Jumatatu, zoezi ambalo awali walitangaza kuwa lingefanyika leo