Sven ampika nyota timu ya vijana

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 May 2020
Sven ampika nyota timu ya vijana

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, anataka kuhakikisha safu yake ya ushambuliaji haipati changamoto baada ya kuzidi kumnoa straika kinda, Cyprian Kipenye, aliyempandisha kutoka timu ya vijana.

Kipenye ni kati ya wachezaji wa timu ya vijana ya Simba waliofanya vizuri katika Kombe la Mapinduzi mwaka huu huko Zanzibar, hivyo kumvutia kocha huyo na kuendelea kuwepo kikosi cha wakubwa.

Sven anaonekana kumkubali mchezaji huyo kutokana na uwezo wake, hivyo kumuamini na kumjumuisha timu ya wakubwa ambapo kwasasa anafanya nayo mazoezi mwanzo mwisho.

Inaonekana wazi kocha huyo ameona Kipenye ndiye anayeweza kuziba pengo la washambuliaji wakongwe waliopo endapo watapata majeraha au kutaka kuwapumzisha.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma wakati John Bocco alipokuwa majeruhi na baadaye Miraj Athumani kuumia, kocha huyo alipata changamoto katika eneo la mbele na kumfanya achezeshe straika mmoja, Meddie Kagere.

Hali hiyo imetokana na Rashid Juma kuonekana hayupo fiti kama ilivyokuwa msimu uliopita, hivyo kumfanya Sven atumie zaidi viungo kumsaidia Kagere.

Kitendo cha kuamua kumpandisha moja kwa moja Kipenye, ni kuepuka kukutana na changamoto ya kukosa straika anayeweza kumfungia mabao pindi wale wanaotegemewa wanapokosekana.

Katika mazoezi ya kikosi hicho yanayoendelea kwasasa huko Mo Simba Arena, jijini Dar es Salaam, inadhihirisha Sven na msaidizi wake, Seleman Matola, wamepania kuhakikisha kijana huyo anaiva, ukizingatia bado wanakabiliwa na mechi muhimu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’