Sven afunguka hatma ya nyota watatu wa kigeni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 May 2020
Sven afunguka hatma ya nyota watatu wa kigeni

Jana baada ya mazoezi ya asubuhi, kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alipata nafasi ya kuzungumza na wanahabari kufafanua masuala mbalimbali yanayokihusu kikosi cha mabingwa hao wa nchi

Miongoni mwa mambo aliyoyagusia ni hatma ya nyota watatu wa kigeni Clatous Chama, Francis Kahata na Sharaff Shiboub ambao bado hawajarejea nchini kuungana na timu

Sven alisema tayari wameandaa utaratibu kwa Chama na Kahata kuwasili wiki ijayo huku kukiwa na ugumu kwa upande wa Shiboub

"Hatuna wasiwasi na ujio wa wachezaji wetu Clatosu Chama na Francis Kahata, nafikiri wiki ijayo watajiunga nasi. Angalau nchi zao hazina masharti magumu katika suala la usafiri licha ya kuwa bado wamefunga mipaka. Lakini kwa Shiboub huenda tukalazimika kusubiri zaidi kwani masharti ya nchi ya Sudan Kusini ni tofauti," alisema

Aidha Sven amesema kikosi chake kiko kamili pamoja na kukosekana nyota hao, wanaendelea kujiandaa kumalizia mechi zilizobaki kuweza kutetea ubingwa

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’