Kiungo fundi Ibrahim Ajib jana alikumbana na adhabu ya kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck baada ya kuchelewa kufika mazoezi
Kocha huyo mwenye msimamo mkali, hakumruhusu Ajib kufanya mazoezi na wenzake ambao aliwakuta wamenza program
Sven amesema hana tatizo na Ajib, adhabu aliyompa ni kutokana na kuchelewa kwake mazoezini na atajiunga nao siku ya Jumatatu
Baada ya mazoezi ya leo asubuhi, Sven alitoa ufafanuzi kuhusu kukosekana kwa kiungo huyo kipenzi cha mashabiki
"Ajibu alichelewa kuripoti mazoezini, nikiwa kama kocha, ninawajibika kumpa adhabu, hivyo nilimtaka arudi nyumbani, asishiriki nasi mazoezi mpaka siku ya Jumatatu," alisema Sven
ADVERTISE HERE