Serikali imetoa mwongozo wa uendeshaji wa shughuli za michezo wakati huu wa janga la corona ambapo upo uwezekano kuwa huenda mashabiki wataruhusiwa kushuhudia mechi za ligi kuu viwanjani kwa tahadhari
Kulingana na mwongozo huo uliotolewa jana na kusainiwa na Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu na Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh Dk Harrison Mwakyembe, vyama vinavyosimamia shughuli za mchezo vimeagizwa kuhakikisha vinazingatia tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa corona
Aidha kama TFF itaruhusu mashabiki kuingia viwanjani, imetakiwa kuhakikisha mashabiki hao wanakaa umbali wa mita moja kati ya shabiki na shabiki
Ingawa mpango huu utapunguza idadi ya mashabiki ambao wataruhusiwa kuingia viwanjani, lakini ni ahueni kwa mashabi kwani mpango uliotangazwa awali ulielekeza mashabiki 20 (10 kwa kila timu) ambao wangeruhusiwa kuingia viwanjani