Benchi la ufundi la Simba limeongeza dozi ya mazoezi kwa wachezaji ili kuhakikisha wanakuwa tayari pale ligi itakaporejea Juni 13
Pamoja na kuhitaji kushinda angalau mechi nne kuweza kutwaa ubingwa ligi kuu, Simba imepania kushinda taji la FA pia ambalo droo ya hatua ya robo fainali itafanyika leo Ijumaa
Baada ya kuanza mazoezi taratibu juzi, siku iliyofuata kocha wa viungo Adel Zrane aliachiwa kikosi kusimamia mazoezi maalum ya viungo ambayo yalihusisha matumizi ya nguvu
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema hiyo ni moja ya program waliyoweka ili kurejesha utimamu wa miili ya wachezaji baada ya wamekaa nyumbani kwa zaidi ya miezi miwili bila ya kucheza mpira
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Sven Vandenbroeck alipendekeza angalau timu kupewa wiki tatu za kufanya mazoezi, pendekezo ambalo limeonekana kuzingatiwa na TFF na Bodi ya Ligi ambao wametangaza ligi itarejea Juni 13