Mabingwa wa nchi Simba wanakaribia kutetea taji lao kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya Bodi ya Ligi kutangza kuwa Juni 13 mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom itarejea kumalizia mechi zilizobaki
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo jioni ya leo Alhamisi, Ratiba ya mechi itatolewa siku ya Jumapili, May 31 2020
Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi katika angalau michezo minne tu kati ya 10 iliyobaki ili kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo
Mechi hazitakuwa nyepesi
Katika hatua nyingine, nahodha wa Simba John Bocco amesema mechi zilizobaki zitakuwa na ushindani kuliko wengi wanavyoweza kufikiria
Bocco amesema ushindani wa mechi hizo utatokana na mazingira ya baadhi ya timu ambazo ziko katika hatari ya kuteremka daraja
Hata hivyo Bocco amesema timu za Dar es salaam zitakuwa na faida ya kucheza mechi zao nyumbani huku timu za kutoka mikoani zitakosa 'uwenyeji' katika mechi zao
Β