Sven ataka kikosi cha wachezaji 25 msimu ujao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 May 2020
Sven ataka kikosi cha wachezaji 25 msimu ujao

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema msimu ujao atahitaji kikosi cha wachezaji 25 ambao atafanya nao kazi msimu mzima

Sven amesema miongoni mwa wachezaji hao, atahitaji wachezaji 20 wazoefu, wachezaji wawili kutoka timu ya vijana na walinda lango watatu

"Sina uhakika na idadi ya wachezaji ambao tutawasajili lakini jambo muhimu ni kuwa nahitaji kuwa na kikosi cha wachezaji 25 msimu ujao," amesema

"Sio zaidi ya wachezaji 20 wenye uzoefu, wawili kutoka timu ya vijana na magolikipa watatu"

Aidha akizungumzia mipango ya kikosi chake kumaliza msimu, Sven amesema wamejiwekea malengo ya kushinda mataji yote mawili yaani ligi kuu na kombe la FA

Hata hivyo amekiri kuwa watahitaji kupambana kushinda FA wakati ubingwa wa ligi kuu hana wasiwasi wako kwenye nafasi nzuri kuubakisha Msimbazi

"Tunahitaji kushinda angalau michezo minne kutwaa ubingwa wa ligi kuu, tunaongoza kwa alama 17 dhidi ya timu inayotufuata (Azam Fc) hivyo tuko na nafasi nzuri ya kutetea ubingwa. FA bado tutakuwa na ushindani na timu nne zilizo nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi, tutahitaji kupambana," aliongeza Sven

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’