Wadau waomba idadi ya mashabiki iongezwe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 May 2020
Wadau waomba idadi ya mashabiki iongezwe

Baadhi ya wadau wa klabu ya Simba wameiomba Serikali kuangalia upya mpango wa kuruhusu mashabiki 20 tu kuingia uwanjani kuzishangilia timu zao wakati ligi itakaporejea

Tayari Serikali imetangaza kuwa ligi itarejea huku mechi zikichezwa bila ya mashabiki lakini wakitoa ruhusa maalum ya mashabiki 10 kwa kila timu kuingia uwanjani kuzishangilia timu zao

Mwenyekiti wa Tawi la Wekundu wa Msimbazi, Ubungo Terminal Justine Joel amesema idadi hiyo ni ndogo sana, anapendekeza angalau mashabiki 300 waweze kuruhusiwa

"Wangeweza kuruhusu makundi matatu ya Ngoma kwa kila timu ambayo kila kundi linakuwa na mashabiki 50 hivyo kufanya idadi ya mashabiki 300 ambao hawatasababisha mkusanyiko kwani wanaweza kukaa katika umbali unaopendekezwa," amesema

"Ugonjwa huu wa corona upo na wataalam wanasema tutaendelea kuishi nao kwa muda mrefu hivyo ni vyema tukaendelea na maisha yetu lakini muhimu tuchukue tahadhari kama inayoelekezwa na wataalam wa Afya"

Simba ndio klabu ambayo inaongoza kwa kuingiza mashabiki wengi kwenye michezo yake na hakika itaathiriwa kwa kiasi kikubwa na uamuzi huu wa Serikali ambao hata hivyo imelazimika kuchukuliwa ili kuepusha maambukizi ya ugonjwa wa corona

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
46m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’