Kagere awakumbuka mashabiki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 May 2020
Kagere awakumbuka mashabiki Simba

Meddie Kagere 'bull-striker' mwamba kutoka nchini Rwanda tayari yuko katika ardhi ya Tanzania akitua nchini kwa usafiri wa barabara baada ya Serikali ya Rwanda kuwa bado imesitisha safari za anga

Leo Kagere anafanyiwa vipimo vya Afya na kama hatakuwa na tatizo lolote ataingia kambini na wachezaji wengine ambao tayari wameanza kuwasili kambini kwa ajili ya zoezi hilo

Kagere amesema ni faraja michezo kurejea baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na janga la corona

Lakini ligi kurejea bila ya mashabiki kutawanyima fursa ya kufurahi na mashabiki wao ambao siku zote wamekuwa nao bega kwa bega kwenye kila mechi

"Kwa kweli tutawakumbuka sana mashabiki wetu kwani tumekuwa nao kila mchezo wakija kwa wingi uwanjani. Tuliwahitaji sana lakini ni muhimu kulinda afya ya kila mmoja wetu kutokana na ugonjwa huu wa corona," alisema Kagere

Kagere anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa amefunga mabao 19, amesema ana matumaini kikosi chao kitarejea na nguvu waliyomaliza nao ingawa watahitaji angalau mechi mbili au tatu kuwa katika kiwango kilichozoeleka

"Hatukuwa pamoja kwa zaidi ya miezi miwili. Kiafya tunaweza kuwa sawa kwani tulikuwa tukifanya mazoezi lakini kitimu pengine tutahitaji muda kidogo kurejea katika mwendo uliozoeleka"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’