Mwongozo shughuli za michezo tayari, kutolewa kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 May 2020
Mwongozo shughuli za michezo tayari, kutolewa kesho

Siku ya Jumatano, May 27 2020, Serikali inatarajia kutoa muongozo kwa kushughuli zote za michezo, ikiwemo ile ya Ligi Kuu na mingine itakavyofanyika bila kuathiri kanuni za afya.

Muongozo huo utatolewa baada ya shughuli zote za michezo kuruhusiwa kufanyika baada ya kusimamishwa kwa takribani miezi miwili kuanzia Machi 17 kupisha janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona kufuatia kuripotiwa kuingia nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo (BMT) Dk Yussuph Singo, alisema muongozo huo ni wa michezo yote na utajumuisha masuala ya kiafya utatolewa baada ya kufanya kikao kilichojumuisha Wizara ya Afya na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

"Tumeshafanya kikao ambacho kimetengeneza muongozo, ambao umejumuisha masuala ya afya na mambo ya kiufundi ya michezo, tumeshakamilisha tunasubiria muongozo upitiwe kwenye mchakato wa kawaida na baada ya hapo utapitiwa na wakuu wa wa wizara zote mbili na kutolewa siku ya Jumatano, "alisema.

Alisema wataanza kutoa muongozo wa jumla kwa michezo yote na baada ya hapo wataanza kutoa kwa kila mchezo ili kuhakikisha kila upande mchezo unafanyika na kuzingatia tahadhari stahiki za kujikinga na janga la virusi vya corona.

Alisema kwenye kikao hicho waliwashirikisha pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi kama ili kupata maoni yao kwakuwa mchezo wa mpira wa miguu una mambo mengi, ikiwemo kuhusisha idadi kubwa ya mashabiki.

"TFF tuliwaita pamoja na Bodi ya Ligi kwakuwa mpira wa miguu una mambo mengi kwanza kuna mechi zimebaki, pili unakusanya idadi ya mashabiki wengi uwanjani"

Muongozo huo unatarajiwa kutolewa baada ya Rais Dk John Magufuli kuruhusu shughuli zote za michezo kuendelea kuanzia Juni Mosi kwa kuwa ni sehemi ya burudani na utasaidia kuondoa hofu kwa baadhi ya watu dhidi ya ugonjwa wa corona.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’