Sven kuwapa nafasi nyota wanaokosa namba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 May 2020
Sven kuwapa nafasi nyota wanaokosa namba

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameahidi kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao wamekosa namba kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo kwenye kikosi hicho

Kimahesabu Simba itahitaji alama 14 kuweza kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo. Ikiwa imebaki na mechi 10, ushindi katika michezo mitano, utatosha kuwapa ubingwa miamba hao wa soka ukanda huu wa Afrika Mashariki

Kocha huyo Mbelgiji amesema atahakikisha wanafanikiwa kutetea ubingwa wao, huku akiamini timu hiyo itakuwa na nafasi ya kuwatumia nwachezaji wengine ambao hawakutumika sana msimu huu

Aidha Sven ameeleza kufurahishwa na uamuzi uliochukuliwa na Mamlaka kwa kuagiza mechi zote kupigwa katika kituo kimoja

Amesema uamuzi huo utakuwa na faida kwa timu ambazo zitakuwa nyumbani lakini pia ni uamuzi sahihi katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya corona

Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 71, alama 17 zaidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 54

Mabingwa hao wa nchi pia wako hatua ya robo fainali michuano ya kombe la FA. Juzi Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa akibainisha kuwa wanalitaka kombe hilo pia

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’