Wakati mabingwa wa nchi Simba, wakitarajiwa kurejea mazoezini siku ya Jumatano, jopo la madaktari wa timu hiyo wamejipanga kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuwapima wachezaji afya
Juzi Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alisema watawapima wachezaji Afya ili kujiridhisha na hali yao kabla ya kuwaruhusu kuanza mazoezi
Aidha kutakuwa na ungalizi maalum kwenye viwanja vya mazoezi ili kuhakikisha hakuwi na mikusanyiko
Maelekezo zaidi kuhusu utaratibu ambao unapaswa kufuatwa na vilabu yanatarajiwa kutolewa na Serikali ambapo uongozi wa Simba umesema unasubiri maelekezo hayo
Simba vinara wa ligi kuu wakiwa wamejikusanyia alama 71, wamepania kumaliza viporo vilivyobaki ili kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo
Lakini pia wakiwa wametinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho, wamepania 'kusepa' na taji hilo pia