Serikali yandaa mkakati wa tahadhari ligi ikirejea

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 May 2020
Serikali yandaa mkakati wa tahadhari ligi ikirejea

Serikali, Bodi ya Ligi (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), juzi walikutana na kujadili utaratibu utakaotumika ili kudhibiti virusi vya Corona ligi zitakaporejea kuanzia Juni 01

Kikao hicho kilizikutanisha Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Afya pamoja na viongozi wa TFF na wa Bodi ya Ligi, kilifanyika katika Ofi si za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizopo Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo alisema kikao hicho kilikuwa maalum kujadili vitu ambavyo vitahitajika kwa wanamichezo na mashabiki katika wakati huu wa kupambana na Virusi vya Corona, licha ya kuwa TFF na TPLB walikaribishwa kusikiliza mchakato huo ili na wao wajue wanaisaidia vipi Serikali wakati michezo hiyo itakapoanza.

"Kikao chetu kilikuwa maalum kujadili misingi ya kiafya itakuwaje pindi ligi itakapoanza. Tumejadili muundo ambao utakuwa sahihi kuutumia ambao utakuwa unazilinda klabu, wachezaji na mashabiki wakati wa ligi

"TFF na BMT wao tulikaribisha kuja kusikiliza kile ambacho sisi tunakijadili, wao ndio wasimamizi wakuu hivyo watapaswa kuzingatia malekezo yote yakayotolewa, " alisema Singo.

Kwa sasa Serikali tayari imeviruhusu vilabu kuanza mazoezi ya pamoja chini ya utaratibu maalum wa kiafya

Bodi ya ligi inatarajiwa kuweka hadharani ratiba ya mechi zilizobaki baada ya sikukuu ya Eid El Fitri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’