Simba kurejea mazoezini Jumatano

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 May 2020
Simba kurejea mazoezini Jumatano

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kuwa kikosi cha timu hiyo kitarejea rasmi mazoezini siku ya Jumatano ijayo baada ya sikukuu ya Eid El Fitri

Akizungumza kupitia ukurasa wa Youtube wa klabu ya Simba, Mtendaji Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Senzo Mazingisa amesema wamepokea kwa furaha uamuzi wa Serikali kurejesha ligi kuu

Senzo amesema lengo lao ni kuhakikisha wanashinda taji la ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la FA

Amesema wachezaji wa kigeni ambao wako nje ya nchi wameendelea kuwasiliana nao kuangaliwa utaratibu wa kuwarejesha mapema huku akibainisha mmoja wa nyota hao atawasili nchini Jumatatu

"Tunafurahi kwamba mpira umerudi kuanzia Juni 1, 2020 .Tumeanza mipango yetu na tumepanga kuanza mazoezi Jumatano baada ya Eid," alisema Senzo

"Wachezaji wetu wote ambao wapo nje ya Tanzania tunawasiliana nao na mmoja kati ya wachezaji hao atakuwepo nchini Jumatatu. Wengine tunatarajia watakuwepo nchini kabla hatujaanza mazoezi."

Aidha kuhusu masuala ya usajili, Senzo amesema mashabiki wawe na subira wakati uongozi ukikamilisha baadhi ya masuala ikiwemo kuwaongezea mikataba wachezaji wanaoendelea kubaki na Simba

"Mashabiki wetu watupe muda na nafasi kufanya kazi nzuri kwenye usajili. Tunaendelea kufanyia kazi kwa wachezaji waliopo kuongeza mikataba mipya na mchezaji yoyote ambaye tutamsajili tutatoa taarifa. Kwasasa hatujasajili mchezaji yeyote."

Simba yazindua tovuti ya klabu

Katika hatua nyingine, uongozi wa klabu ya Simba umeitambulisha tovuti rasmi ya klabu ambayo itakuwa ikitoa taarifa muhimu za klabu pamoja na matukio mengine yanayowahusu mabingwa hao wa nchi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’