Simba yapambana kuwarejesha Chama, Kahata

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 May 2020
Simba yapambana kuwarejesha Chama, Kahata

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, amefunguka kuwa wanaendelea na jitihada za kuwapata wachezaji wao, Francis Kahata na Clatous Chama ambao wapo nje ya nchi kwa ajili ya kumalizia mechi zao zilizobakia za Ligi Kuu Bara

Senzo amesema kuwa wanaendelea kuwasiliana na wachezaji hao kwa ajili ya kuwarejesha Bongo kuendelea na majukumu yao kwenye kikosi hicho.

Chama, Kahata, Meddie Kagere na Sharaf Shiboub ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wapo kwao baada ya kuondoka mwanzoni mwa mwezi uliopita kwa ajili ya kuzitumikia timu zao za taifa.

Bosi huyo wa Simba amesema kuwa amekuwa na mawasiliano na wachezaji hao kwa ajili ya kuwarudisha nchini ambapo kwa sasa imekuwa ngumu kwa wachezaji hao kurejea kutokana na mipaka ya nchi za Zambia na Kenya kufungwa

"Tunawasiliana nao wachezaji wote ambao wapo nje na mimi nimekuwa nikiongea nao kila mara kuhusiana na jambo hilo.

"Tunawasiliana nao kuona wanarudi kwa wakati ili waje kumaliza kazi ambazo zimebaki lakini inakuwa ngumu kwa sababu baadhi yao hawawezi kutoka kwani bado ndege haziruhusiwi kutoka kwenda sehemu nyingine," Senzo aliliambia gazeti la Championi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
38m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’