Klabu ya Simba imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake kisiki Paschal Wawa, imefahamika
Wawa ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye majadiliano ya kuhuisha mikataba kama ilivyokuwa kwa Said Ndemla, Hassan Dilunga na Deo Kanda
kanda, Dilunga na Ndemla wao walisaini mikataba mipya wiki iliopita huku mkongwe huyo akimwaga wino mwanzoni mwa wiki
Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema wanaendelea kuhuisha mikataba ya nyota wao waliopendekezwa na kocha Sven Vandenbroeck
Amesisitiza michakato ya usajili wa wachezaji wapya itaanza pale dirisha la usajili litakapofunguliwa
ADVERTISE HERE