Maproo Simba hatarini kukosa mechi za mwanzo ligi ikirejea

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 May 2020
Maproo Simba hatarini kukosa mechi za mwanzo ligi ikirejea

Nyota wa Simba ambao wako nje ya nchi wanaweza kuchelewa kurejea nchini kutokana na vikwazo ambavyo viko katika nchi zao licha ya Serikali ya Tanzania kuruhusu usafiri wa anga

Inaelezwa wakati wowote ligi inaweza kurejea kumalizia mechi zilizobaki baada ya Rais Dk John Magufuli kuahidi kuwa anaweza kutoa ruhusa hiyo wiki hii

Nyota watano wa Simba bado wako nje ya nchi wakisubiri maelekezo zaidi katika nchi zao ambazo baadhi zimefunga mipaka huku nyingine zikiwa bado hazijaruhusu usafiri wa anga

Kinara wa mabao ligi kuu ya Vodacom Meddie Kagere, ni miongoni mwa wachezaji hao ambao wanasubiri ruhusa katika nchi zao

Rwanda bado haijaruhusu usafiri wa anga pamoja na kuwa huenda ruhusa hiyo ikatolewa karibuni baada ya nchi hiyo kuanza kuondoa lockdown

Nyota wengine ambao wako nje ni Clatous Chama (Zambia), Luis Miquissone (Msumbiji), Sharaff Shiboub (Sudan) na Francis Kahata (Kenya)

Wachezaji hao watakaporejea pia watakaa karantini kwa siku 14

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wako tayari kupambana kumalizia mechi zilizobaki hata ikitokea wachezaji hao watachelewa

Matola amesema wanasubri ruhusa ya Serikali ili kuwaita wachezaji kambini kuanza maandalizi

Amesema wataandaa timu kulingana na wachezaji watakaokuwepo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’