Wekundu wa Msimbazi Simba, wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba.
Mchezo huo ulikuwa wa kisasi kwa Simba baada ya kupoteza mchezo uwanjani hapo msimu uliopita na kuvurugiwa hesabu za ubingwa.
Mabao yote ya Simba yalipatikana kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Said Khamis Ndemla (69') na John Bocco (80') aliyetengenezewa na Shomari Kapombe aliyerejea dimbani kwa mara ya kwanza leo baada ya kuwa nje kwa miezi mitano.
Ushindi huo umeirejesha Simba kileleni baada ya kufikisha alama 32 na kuiondoa Azam FC yenye alama 30.
Nayo Singida United imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Majimaji katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 14

ADVERTISE HERE