Kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya amesema anajiandaa kuitumikia timu hiyo kikamilifu baada ya kumaliza changamoto zilizokuwa zikimkabili
Kichuya aliyerejea Simba mwezi Januari akitokea klabu ya Pharco Fc, amesema kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara huko Misri kulipelekea kuongezeka uzito
Aidha Kichuya amebainisha kuwa alilazimika kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kutokea sintofahamu
"Nilipokuwa Misri sikuwa nikipata nafasi ya kucheza mara kwa mara, kulitokea sintofahamu ambayo ilinikosesha mazoezi na timu kwa zaidi ya miezi saba na ndiko kulikonipelekea mimi kuongezeka uzito"
"Kwa sasa nashukuru nimepungua sana uzito na najipanga kurejea kwenye ubora wangu," amesema Kichuya
Kichuya alisajiliwa sambamba na Luis Miquissone, hata hivyo wakati Mmakonde huyo akijihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza, kwa Kichuya imekuwa tofauti
Ligi itakaporejea atakuwa na nafasi ya kudhihirisha thamani yake