Nchi ya Uganda imekuwa ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya wakitangaza kumaliza msimu wao kutokana na janga la corona
Shirikisho la soka la nchi hiyo (FUFA) limetangaza uamuzi wa kufuta msimu leo huku wakiwapa ubingwa Vipers wakitumia matokeo ya mechi zinazokamilisha robo tatu ya msimu
Kwa upande wa nchi nyingine Afrika Mashariki, Tanzania Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) linasubiri ruhusa ya Serikali kuweka gozi uwanjani kumalizia ngwe iliyobaki wakati Burundi wao ligi yao itaendelea mwezi Juni
Nchi ya Rwanda bao haijaweza hadharani mkakati wake lakini zipo dalili kuwa nao watamalizia msimu kama ilivyo kwa Tanzania na Burundi
ADVERTISE HERE