TPLB yajadili utaratibu wa kurejesha Ligi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 May 2020
TPLB yajadili utaratibu wa kurejesha Ligi

Bodi ya Ligi imesema inajadili utaratibu watakaoutumia kumaliza mechi 90 za ligi kuu zilizobaki ili kukamilisha msimu

Kumekuwa na hoja kinzani kuhusu utaratibu ambao unapaswa kufuatwa kukamilisha msimu ambapo baadhi ya wadau wamependekeza mechi zipigwe katika kituo kimoja huku wengine wakipendekeza utaratibu wa kawaida wa mechi kuchezwa nyumbani na ugenini utumike

Mwenyekiti wa Bodi hiyo Steven Mguto amesema watatoa uamuzi wa pamoja baada ya kufikia mwafaka lakini amekiri wanaangalia uwezekano wa mechi hizo kupigwa katika kituo kimoja (Dar es salaam) kama timu zote zitaafiki

"Tuna mapendekezo mbalimbali tunayajadili kuona ni vipi tunaweza kukamilisha msimu. Lakini kama timu zote zitakubaliana mechi zichezwe katika kituo kimoja basi hatutakuwa na pingamizi," amesema

Mguto pia amesema wanaangalia uwezekano wa kuvisaidia vilabu ambavyo vimekummbwa na hali tete ya kiuchumi kutokana na janga la corona

Ikumbukwe ligi itakaporejea mechi zote zitapigwa bila ya uwepo wa mashabiki na kama utaratibu wa mechi kupigwa nyumbani na ugenini utatumika, ni wazi timu zitapaswa kuwa na fedha kuweza kusafiri pamoja na kugharamia kambi kila wanapokwenda

Mguto amezitaka timu ziwe na subira kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali, wakati sahihi wa ligi kurejea utakapotangazwa na Serikali, wao wako tayari

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’