Kagere tayari kurejea kuendeleza 'shoo za kibabe'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 May 2020
Kagere tayari kurejea kuendeleza 'shoo za kibabe'

Mshambuliaji wa Simba kinara wa mabao Meddie Kagere anatarajiwa kurejea wiki hii baada ya Rais wa nchi Dk John Magufuli kutangaza kuwa huenda akaruhusu safari za anga baada ya maambukizi ya corona kupungua

Kagere, kinara wa mabao ligi kuu ya Vodacom akiwa na mabao 19, alikwama kwao nchini Rwanda alikokuwa amekwenda kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa

Ni baada ya Serikali ya Rwanda kufunga mipaka na kuzuia usafiri wa anga huku ikiweka lock-down kwa wananchi wote

Hata hivyo kama ilivyo Tanzania, Rwanda nayo imeanza kulegeza masharti wakiwa tayari wameondoa lock-down na watu kuanza kurejea katika shughuli zao

Aidha upo uwezekano mkubwa ligi kuu ya Vodacom itarejea mwanzoni mwa mwezi Juni

Kuruhusiwa kwa safari za anga nchini kumewapa ahueni nyota wa Simba waliokwama kwenye nchi zao kutokana na corona

Wachezaji wengine wa Simba ambao wako nje ya nchi ni Clatous Chama, Sharaff Shiboub, Francis Kahata na Luis Miquissone

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
17h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
20h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’