Simba yajitosa kumuwania nyota Rayon Sports

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 May 2020
Simba yajitosa kumuwania nyota Rayon Sports

Tetesi zilizoibuliwa viungani leo ni uwepo wa taarifa ya mabingwa wa nchi Simba kujitosa kumuwania mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports Michael Sarpong

Nyota huyo raia wa Ghana yuko huru baada ya klabu ya Rayon kuvunja mkataba wake mwezi uliopita kufuatia matamshi yake ambayo aliyatoa kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari huko Rwanda

Nyota huo alikuwa akipinga uamuzi wa klabu hiyo kuwakata wachezaji mishahara baada ya timu kukumbwa na changamoto za kiuchumi kutokana na janga la corona

Sarpong mwenyewe amethibitisha kufanya mazungumzo na mmoja wa viongozi wa Simba

Wiki iliyopita ziliibuliwa tetesi klabu ya Yanga kupitia wadhamini wao GSM nao walijitosa kumuwania mshambuliaji huyo ambaye mpaka ligi ya Rwanda inasimama, alikuwa amefunga mabao nane

Sarpong ni mmoja wa washambuliaji hatari kwenye ligi kuu ya Rwanda akiwa amefunga jumla ya mabao 24 katika misimu yake miwili kwenye ligi hiyo

Simba inatarajiwa kusajili mshambuliaji mmoja wa kati ambaye atawapa 'back-up' Meddie Kagere na John Bocco

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’