Kiungo Said Khamis Ndemla yuko mbioni kusaini mkataba mpya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa nchi, imefahamika
Ndemla ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha Sven Vandenbroeck alipendekeza apewe mkataba mpya
Siku za karibuni kuliibuka mjadala mkali kwa baadhi ya wadau kumshauri kiungo huyo aondoke Simba kwa kuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Hata hivyo Ndemla ambaye yuko Smba tangu mwaka 2012, aliwataka wote wanaomshauri kuhusu mustakabali wake na Simba watulie kwa kuwa ni yeye mwenyewe anayefahamu ni kitu gani anataka
Inaelezwa tayari mazungumzo ya kumuongeza mkataba yamekamilika na atasaini mkataba wa miaka miwili
Kabla ya kufikia uamuzi wa kuongeza mkataba Simba, Ndemla alikuwa akifuatilia 'mchongo' wa kwenda nchini Sweden kataia moja ya vilabu ambavyo alifanya majaribio na kufuzu