Mfumo haumsumbui Okwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jan 2018
Mfumo haumsumbui Okwi
Wakati leo wakishuka kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuumana na wenyeji Kagera Sugar, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, ameweka wazi kuwa yupo tayari kucheza katika mfumo wowote ambao kocha wa timu hiyo ataamua kuutumia.

Simba kwa siku za karibuni imekuwa ikitumia mfumo wa 3-5-2 chini ya aliyekuwa kaimu kocha mkuu, Masoud Djuma, ambaye ameipa ushindi kwenye michezo yote miwili ya Ligi Kuu aliyokiongoza kikosi hicho.

Tayari Simba imeajiri Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre, ambaye sasa anarithi mikoba ya Mcameroon Joseph Omog aliyetimuliwa, jambo ambalo kocha huyo anaweza kuja na mfumo mpya.

Katika mahojiano na gazeti la Nipashe, Okwi, amesema kuwa yeye kama mchezaji yupo tayari kufuata na kuyashika maelekezo ya kocha wake kulingana na mfumo atakoupendekeza.

"Wachezaji wote tupo chini ya kivuli kimoja ambacho ni kocha, kwa namna yoyote ambayo ataona ni vema sisi kucheza, tutafanya hivyo, sihofii mfumo wowote, nipo tayari kucheza katika namna ambayo kocha atataka," alisema Okwi.

Aidha, alisema kuwa anataka kutuliza akili kwenye timu katika michezo yote iliyobakia kabla ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu.

"Nataka niwatoe hofu mashabiki na wapenzi wa Simba, nipo kwa ajili ya kuitumikia timu hii ambayo kwangu naiheshimu sana, nimerudi na kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu tutahakikisha tunapambana kuipa timu ubingwa,"alisema Okwi.

Mshambuliaji huyo raia wa Uganda anaongoza kwa mabao kwenye Ligi Kuu baada ya kutupia mara 10, mawili akiyafunga kwenye mchezo dhidi ya Singida United wiki iliyopita.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’