Sven awabadilishia mazoezi wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 May 2020
Sven awabadilishia mazoezi wachezaji Simba

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewabadilishia program ya mazoezi wachezaji wake ili kuhakikisha wanakuwa tayari kwa ajili ya lala salama ligi kuu ya Vodacom

Vinara hao wa ligi kuu wanasubiri kipenga cha ngwe ya mwisho kipulizwe ili waondoke na 'ndoo' yao ya tatu mfululizo

Juzi benchi la ufundi likiongozwa na Sven kwa kushirikiana na madaktari wa Simba, waliendesha program ya kuwapima uzito wachezaji

Huu ni utaratibu ambao Simba iliweka ili kujiridhisha na maendeleo ya wachezaji katika kufanya mazoezi hasa wakati huu ambao wanafanya mazoezi binafsi kutokana na corona

Vipimo vya baadhi ya wachezaji vilionyesha kupungua uzito jambo ambalo ni ishara walikuwa wakifanya mazoezi zaidi ya kiwango walichotakiwa

"Kocha ametoa program nyingine ya mazoezi, katika kuhakikisha wachezaji wanakuwa tayari wakati wowote ligi itakapotangazwa kurejea. Mwalimu ameridhishwa na mwenendo wa wachezaji katika mazoezi, kikubwa amewataka kuzingatia zaidi kufanya mazoezi wanayoelekezwa," alisema Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu

Mikiki mikiki ya ligi huenda ikarejea mwezi katikati ya mwezi Juni, kutegemeana na jinsi Serikali itakavyoelekeza

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’