Serikali yasisitiza Mo apewe hisa asilimia 49

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jan 2018
Serikali yasisitiza Mo apewe hisa asilimia 49
Wakati Mohamed "Mo" Dewji, akiendelea kuiimarisha Simba, kufuatia kushinda tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam, Serikali imetoa msisitizo kwa 'Wekundu wa Msimbazi' hao kuzingatia sheria na kanuni zinayosimamia suala la uwekezaji kwa klabu zilizoanzishwa na wanachama, kutakiwa kumiliki asilimia 51 na mwekezaji 49.

Msisitizo huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50 kwa mwekezaji wa klabu hiyo, Dewji waliyemtangaza hivi karibuni ambapo ni kinyume cha sheria.

Ò€œKanuni zinazosimamia masuala ya udhamini kwa klabu zilifanyiwa marekebisho Novemba 2017 na ilionekana ni vyema klabu za michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata mwekezaji, basi achukue asilimia 49 na wanachama kutokana na mchango wao mkubwa kwa klabu basi wapewe asilimia 51, lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,Ò€Dk. Mwakyembe.

Mwakyembe alisema serikali ya awamu ya tano haijaja kuua michezo, bali lengo lake ni kuboresha michezo na kuifanya kuwa na tija zaidi pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hiyo.

Naye Katibu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Mohamed Kiganja, alieleza kuwa ofisi yake ipo katika maandalizi ya kuwaandikia barua Klabu ya Simba kuipa msisitizo wa serikali katika kuzingatia sheria kwenye suala la udhamini na barua hiyo itawafikia wiki ijayo.

Kwa upande wa Kaimu Rais wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah, alieleza vyombo vya habari kuwa wanashukuru serikali kwa kuwaeleza kuwa milango iko wazi pale watakapokuwa na tatizo au watakapohitaji ushauri wanaweza kuonana na watendaji wake.

Kwa muda mrefu Mo ameelezwa kuisaidia Simba na ndiye anayedaiwa kumleta na kocha mpya, Mfaransa Pierre Lechantre.

IPP Media
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
16h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
20h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’