Beki wa Simba raia wa Brazil Tairone Da Silva amesema amewakumbuka mashabiki wa timu hiyo hasa shamrashamra zao pale timu inapokuwa imepata matokeo
Tairone amesema wamekaa muda mrefu bila kuwaona mashabiki wao hivyo wana shauku kubwa na kusubiri kwa hamu ligi irejee
Beki huyo mrefu amesema, anataka kutwaa ubingwa wa msimu huu akiwa na kikosi cha Simba
"Nimewakumbuka mashabiki wetu na kushangilia ushindi pamoja na wachezaji wenzangu. Nataka kushinda ubingwa nikiwa na Simba," amesema
Tairone ni mmoja wa wachezaji watatu raia wa Brazil waliosajiliwa na Simba msimu huu
Wakati mshambuliaji Wilker Da Silva 'alichemsha' na kuondoka usajili wa dirisha dogo, Tairone na Gerson Fraga wao bado wanaendelea kutamba ndani ya uzi wa rangi nyekundu na nyeupe
ADVERTISE HERE