Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TFF) imeeleza kuchunguza matumizi mabaya ya fedha ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati wa michuano ya AFCON U17 iliyofanyika nchini mwaka uliopita
Fedha hizo ni zile Bilioni moja zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ili kufanikisha michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza hapa Tanzania
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig John Mbungo amesema wanaendelea na uchunguzi pamoja na kuwahoji wahusika
Amesema wahusika wana hiari ya kurudisha fedha hizo kabla hatua stahiki hazijachukuliwa dhidi yao uchunguzi utakapokamilika
ADVERTISE HERE