TFF yafunguka kuhusu mabilioni ya FIFA

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 May 2020
TFF yafunguka kuhusu mabilioni ya FIFA

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeta ufafanuzi juu ya pesa zinazotolewa na Shirikisho la mpira duniani (FIFA) katika kipindi hiki cha janga la Corona kutokana na upotoshaji unaendelea katika baadhi ya vyombo vya Habari hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya Habari kwa njia ya mtandao, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema pesa hizo Dola 500,000 sawa na shilingi bilioni 2.3 zinatolewa kwa ajili ya masuala ya kiundeshaji na haziwezi kuzitumia nje ya maelekezo ya FIFA.

Kidao amesema pesa hizo watazitumia katika kuwalipa waamuzi stahiki zao, kulipigia gharama za timu za Taifa ambazo walicheza mechi 17 kabla ya Corona kuingia, mishahara ya watumishi.

Kidao ameongeza kuwa kuna baadhi ya nchi zilitangaza kuwa zitagawa kiasi hicho cha pesa kwa timu shiriki lakini wameulizia inapita wiki mbili sasa lakini hazijalipwa kwakua haiwezekani kutokana gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

"Hizi pesa zinatolewa kwa uwazi na FIFA lazima wazifuatilie matumizi yake. Kabla ya pesa kuingia FIFA wanatumia barua kwanza ya jinsi ya kuzitumia na kama ukienda kinyume unafungiwa unakuwa hupati kama ilivyotokea katika uongozi uliopita.

"TFF chini ya Rais Wallace Karia imekuwa wazi kama ilivyo jipambanua katika uchanguzi Mkuu na hata FIFA wenyewe wamekuwa wakitupongeza kwa jinsi tunavyo simamia matumizi ya pesa lakini tunashangaa kusikia watu wanakaa vijiweni wanazungumza vitu ambavyo hata hawavijui," alisema Kidao.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’