Wanachama Simba kuandikishwa kidigitali

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 May 2020
Wanachama Simba kuandikishwa kidigitali

Uongozi wa klabu ya Simba uko kwenye hatua za mwisho kuandaa kanzi data ambayo itahifadhi taarifa za Wanachama wote wa klabu hiyo

Mkurugenzi wa Wanachama na mashabiki Hashim Mbaga amesema kupitia utaratibu huo, watakuwa na taarifa sahihi ya idadi ya Wanachama na mashabiki wao

"Tunataka kuachana na huu utaratibu wa kukisia idadi halisi ya wanachama wetu, ndio maana utaratibu huu umetengenezwa kutuwezesha kuwa na takwimu sahihi," amesema

"Zoezi la kwanza tutapita mikoa yote kuhakiki wanachama kwa kuchukua taarifa zao sahihi zikiwemo picha na namba zao za simu pamoja na kubaini wanachama ambao hawajalipa ada zao"

"Baadae tutapita kwenye matawi yetu kufahamu idadi halisi na kwa Matawi ambayo yatakuwa hajaandikishwa, kutakuwa na zoezi la uandikishaji"

Mbaga ameongeza kuwa kanzi data hiyo itarahisisha mawasiliano kati ya uongozi wa Simba na Wanachama wake kwani taarifa zote muhimu zitakuwa zikitumwa moja kwa moja kwa Wanachama ambao wameandikishwa kwenye mfumo

Mfumo huo pia utaiwezesha klabu ya Simba kunufaika kutokana na wingi wa Wanachama na mashabiki wake kupitia ukusanyaji wa ada mbalimbali pamoja na mauzo ya bidhaa za klabu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’