Hatutadharau mechi - Rweyemamu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 May 2020
Hatutadharau mechi - Rweyemamu

Wakati wadau wakisubiri Serikali ipulize kipenga cha kurejea ligi kuu ya Vodacom kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki, Meneja wa klabu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema, wamejipanga kukamilisha ligi hiyo kwa kishindo

Kimahesabu, Simba inahitaji kushinda mechi tano tu kuweza kutwaa ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo kutoka mechi 10 zilizobaki

Hata hivyo Rweyemamu amesema pamoja na mazingira hayo, amesema hawatadharau mechi ili kuhakikisha wanakamilisha lengo lao

Rweyemamu amesema mechi za lala salama mara nyingi zinakuwa ngumu kutokana na baadhi ya timu kupambana katika jitihada za kujinusu na kuteremka daraja

Amesema uongozi wao wa tofauti ya alama 17 dhidi ya timu inayofuata nafasi ya pili, umewaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa

"Sisi tumebakiza mechi tano tu ili tutangazwe mabingwa wapya kwa msimu wa tatu mfululizo, ingawa tunajua kutakuwa na ugumu katika baadhi ya mechi, hasa ukicheza na timu zinazotaka kujinasua, lakini tumejipanga kuendeleza kuvuna matokeo mazuri," amesema

Aidha Rweyemamu amesisitiza kuwa ili kikosi chao kisipoteze malengo yake, kimejiandaa kurejea kwa kasi ili kusaka matokeo mazuri na haitadharau mchezo wowote wa ligi hiyo na katika mashindano ya Kombe la FA ambayo yameingia kwenye hatua ya robo fainali.

Alisema wachezaji wao wote wanajua wanachotakiwa kukifanya katika hatua ya lala salama na wanaamini huu ni wakati mwingine wa kujiongezea thamani kwa kuonyesha viwango vya juu.

"Jambo ambalo halitulifahamu mpaka sasa ni kujua ligi itarejea katika mazingira gani, lakini hata mazingira hayo hayo tusiyoyajua, tutayapokea kama yatakavyokuwa, changamoto itakuwa katika mechi ya kwanza na ya pili, mechi ya tatu tutakuwa tumeshazoea na maisha lazima yaendelee"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
46m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’