Serikali yadokeza ligi inakaribia kurejea

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 May 2020
Serikali yadokeza ligi inakaribia kurejea

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbasi amesema wako katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kuruhusu ligi kuu ya Vodacom kurejea kumalizia mechi zilizobaki

Dk Abassi amesema juzi Jumatatu walikuwa na kikao cha pamoja na BMT, TFF, TPLB na Rais wa zamani wa TFF Leodegar Tenga kujadili mustakabali wa lig hiyo

"Kikao chetu kilijikita kajadili taratibu ambazo tunapaswa kuzitumia pale Rais Dk Magufuli atakaporuhusu shughuli za michezo kurejea nchini," amesema

Aidha Dk Abassi amesema kama mashabiki wataruhusiwa kuingia viwanjani, wamejadili utaratibu ambao watalazimika kufuata kwa ajili ya tahadhari

Lakini pia wamejadili ni aina gani ya watu watapaswa kuingia viwanjani iwapo Serikali haitaruhusu mashabiki kuingia

Hata hivyo DK Abassi amesema tarehe rasmi ya ligi hiyo kurejea bado haijafahamika lakini amewahakikishia wadau wa soka nchini kuwa Serikali imedhamiria kurejesha ligi hiyo mapema

"Tunataka kuona washindi wa ligi wanapatikana uwanjani na sio vinginevyo," amesema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’