Winga wa Mtibwa Sugar, Salumu Kihimbwa amekiri kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miqussone ni mchezaji anayetumia akili na maarifa anapokaribia eneo la goli la wapinzani na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.
Kihimbwa ambaye huu ni msimu wa tatu akichezea Mtibwa Sugar, akitokea klabu ya Moro United amesema Miqussone ni mbunifu zaidi kwa kipindi alichocheza ameonesha tofauti kubwa na wachezaji wazawa.
Kihimbwa amefichua kuwa walipokutana na Miquissone Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup alijua ni mchezaji wa kawaida na amekuja kumaliza fedha za watu.
"Siku ya pili nilimshuhudia akicheza mchezo wake wa kwanza alitokea benchi nikaona ameonesha kiwango cha kawaida, lakini kadri muda ulivyosogea alizoea mazingira saa hivi nimenyoosha mikono yangu yote miwili juu kuwa ni mchezaji hatari," alisema Kihimbwa.
Alimfananisha kiwango cha Miqussone na kiungo Ibrahim Jeba aliyewahi kucheza Azam Fc na Mtibwa Sugar ambaye ni marehemu kwa sasa.
"Kweli yule mtu anajua soka na anastahili kuitwa mchezaji wa kimataifa ana uwezo mkubwa kama Jeba "alisema Kihimbwa
Kihimbwa amesaliwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake na anakaribisha timu inayomhitaji kujitokeza kuvunja mkataba kwani anatamani kupata changamoto mpya ili kukuza kiwango chake