Uongozi wa klabu ya Simba hauna mpango wa kumuongezea mkataba kiungo wake mshambuliaji Mohammed Ibrahim 'Mo' ambaye msimu huu anaitumikia Namungo Fc kwa mkopo
Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema katika mkakati wao wa usajili msimu huu, wataachana na baadhi ya wachezaji wao ambao waliwatoa kwa mkopo kwenda timu nyingine
Aidha alisema ili kupunguza gharama za kulipa mishahara ya wachezaji ambao hawachezi Simba, kuanzia sasa timu yoyote inayomtaka mchezaji wa Simba kwa mkopo ni lazima iwe na uwezo wa kulipa mshahara wake wote
Mo Ibrahim pamoja na beki Paul Bukaba walitolewa kwa mkopo Namungo na wote watakuwa huru miwshoni mwa msimu pale mikataba yao itakapomalizika
Mo Ibrahim amesema tayari anajiandaa kuondoka Simba akisikilizia ofa kutoka vilabu vingine
Mkataba wangu na Simba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, na kama mambo yakienda vizuri basi nitaondoka hapo na kwenda kwingine kutafuta changamoto mpya.
"Tayari baadhi ya klabu zimenifuata kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kikubwa kujadiliana katika dau la usajili ambalo mimi ninalitaka," amesema
Nyota wengine ambao walitolewa kwa mkopo na mikataba yao inamalizika ni pamoja na Marcel Kaheza (Polisi Tanzania) na Mohammed Rashid (JKT Tanzania)