Mshambuliaji wa Simba Meddie ameweka rekodi ya kufunga mabao 69 katika kipindi cha misimu minne ikiwa ni pamoja na mabao aliyofunga mpaka sasa msimu huu
Kagere alitua Simba mwaka juzi akitokea klabu ya Gor Mahia ambayo aliitumikia kwa misimu miwili
Akiwa Gor Mahia Kagere alifunga mabao 27 idadi ambayo imeongezeka mara dufu alipojiunga na Simba
Kwenye msimu wake wa kwanza na Simba Kagere alifunga mabao 23 na mpaka sasa msimu huu akiwa amefunga mabao 19 hivyo kufanya awe amefunga mabao 42 mpaka sasa
Mwamba huyo aliyezaliwa Rwanda na kukulia UGanda, anaweza kuongeza idadi ya mabao yake pale ligi itakaporejea kwani klabu yake ya Simba bado ina mechi 10 mkononi
ADVERTISE HERE