Kagere awapa mzuka wa mazoezi wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 May 2020
Kagere awapa mzuka wa mazoezi wachezaji Simba

Mshambuliaji wa Simba, raia wa Rwanda, Meddie Kagere, amewatumia ujumbe mzito wachezaji wanzake kuhakikisha wanafanya mazoezi pasipo kuzembea ili Ligi Kuu Tanzania Bara ikirudi waweze kuendeleza moto ule ule.

Kagere na wachezaji wenzake wa kigeni wakiwamo Clatous Chama (Zambia), Luis Miquissone (Msumbiji), Francis Kahata (Kenya) na Sharaf Shaboub (Sudan), wamekwama kurejea nchini, baada ya nchi zao kufunga mipaka kutokana na tishio la maambukizi ya virusi vya corona.

Wachezaji hao walikwenda kwao kujiunga na timu za taifa ambazo zilikuwa zinakabiliwa na michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), ambayo baadaye ilisitishwa na Shirikisho la Soka Afrika kutokana na nchi kukumbwa na corona.

Kutokana na hali hiyo, Serikali ilisitisha shughuli zote za mikusanyiko ya watu, ikiwamo Ligi Kuu Bara inayoelezwa inaweza kuendelea mwezi ujao.  

Hata hivyo, Kagere amesema janga la corona bado ni kubwa lakini wachezaji  wanatakiwa kuendelea kufanya mazoezi kwa lengo la kulinda viwango.

Kagere aliandika katika ukurasa wake wa Instagram na mwenzake Mohammed Hussein kuwa amekuwa akizingatia program maalum ya mazoezi waliyopewa na makocha wao baada ya ligi hiyo kusimamishwa na Serikali Machi 17, mwaka huu.

"Huku kwetu bado hali ni mbaya, nadhani tunahitaji kuendela kutulia nawaombeni tuendelee kujifua kama tuko pamoja, msipuuze mazoezi na itapendeza mkijiongezea ya ziada," aliandika. 

Kagere amekuwa akiwasialiana na mchezjai mmoja mmoja kuhamasisha suala zima la kufanya mazoezi ili watakaporejea waendeleze moto ule ule

Bingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’