Kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miquissone, ameibuka na kusema kuwa anatamani kuona janga la ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na Virusi vya Corona, lipotee ili waweze kurejea uwanjani kupigania ubingwa wao wa msimu huu.
Luis ambaye kwa sasa yupo kwao Msumbiji, amesema amekumbuka sana majukumu yake hasa akifurahia mwanzo mzuri wa maisha yake kunako klabu ya Simba
Miquissone amesema wamebakisha mechi chache waweze kutwaa ubingwa kwa msimu wa tatu hivyo wanasubiri kwa hamu tarehe ya kutangazwa kurejea kwa ligi kuu ili wamalizie mechi zilizobaki kujihakikishia ubingwa
"Nimekuwa nikikumbuka kucheza mpira lakini haiwezekani kwa sababu ya Corona, nafanya mazoezi kutokea nyumbani na kuendelea kujilinda katika kipindi hiki kigumu kwa kuwa ni tatizo ambalo dunia nzima bado haijaweza kulipatia ufumbuzi kitu ambacho kimepelekea kuharibu kila kitu.
"Unajua sisi tunaongoza ligi na matarajio ni kuweza kuchukua ubingwa na ndiyo malengo ya timu lakini Corona imezuia kuendelea na ligi lakini natamani kuona imeisha ili kuweza kurejea uwanjani na kuona tunamalizia mechi zilizobaki kwa ushindi ili tuchukue ubingwa," alisema
Miquissone alijiunga na Simba mwezi Januari katika usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya UD Songo ambayo alikuwa akicheza kwa mkopo kutokea timu ya Mamelodi Sundowns
Mmakonde huyo ameweka kambani mabao matatu kwenye ligi