Beki KCB akaribisha mpango wa kujiunga na Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 May 2020
Beki KCB akaribisha mpango wa kujiunga na Simba

Siku za karibuni ziliibuka tetesi kuwa Simba inaweza kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya KCB na timu ya Taifa ya Kenya Mike Kibwage

Hata hivyo beki huyo kisiki amezisikia tetesi hizo na kubainisha kuwa bado hakuna mazungumzo aliyofanya na viongozi wa Simba lakini atakuwa tayari kujiunga na mabingwa hao wa nchi kama watamfuata

Nyota amesema Simba ni klabu kubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashabiki hivyo itakuwa ngumu kwake kukataa kujiunga nao kama watamuhitaji

"Nimezisikia tetesi nyingi huko Tanzania kunihusu mimi kutakiwa na Simba, lakini kiukweli sijafanya mazungumzo na kiongozi yeyote. Lakini ikitokea wakanihitaji na wakanipatia ofa nzuri siwezi kupinga. Najua Simba ni timu kubwa Tanzania na hapa Afrika Mashariki"

Mkataba wake na klabu ya KCB utamalizika mwezi Oktoba mwaka huu

Simba inatarajiwa kusajili mlinzi mmoja wa kati ambaye atakuja kuwaongezea nguvu walinzi waliopo

Jina la Kibwage ni miongoni mwa majina ambayo yametajwa sana hapo Msimbazi. Walinzi wengine wanaohusishwa na Simba ni mzawa Bakari Nondo Mwamnyeto na Mghana Yacoub Mohammed anayechezea Azam Fc

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’