Ammy Kessy ambaye ni Meneja wa kiungo wa Simba Ibrahim Ajibu amesema kwa sasa anafikiria zaidi kumtafutia mteja wake nafasi nje ya nchi na sio vilabu vya hapa nchini
Kessy amesema hana wasiwasi kuwa Ajibu atapata nafasi kwenye kikosi cha Simba akiamini kukosa nafasi kwake kulisababishwa kwa kiasi kikubwa na changamoto zilizokuwa zikimkabili yakiwemo majeraha ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu
"Wakati kocha mpya (Sven) anaanza majukumu yake Ajibu alikuwa nje ya kikosi kutokana na matatizo ya kifamilia. Aliporejea imekuwa sio rahisi kuingia kwenye kikosi cha ushindi ambacho Sven tayari alikuwa amekiunda. Lakini naamini kwa kipaji alichonacho, nafasi yake ipo. Na akianza kucheza hakuna mchezaji atamuweka benchi," alisema Kessy
Ajibu bado ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi katika kikosi cha Simba
Β